Uchunguzi wa Uundaji wa Vitambulisho Vya Utaifa Katika Tamthilia ya Mstahiki Meya

dc.contributor.authorMargaret June Achieng` Mung`ala
dc.contributor.authorGeorge Obara Nyandoro
dc.contributor.authorCharles Nyandoro Moochi
dc.date.accessioned2025-11-29T19:36:04Z
dc.date.issued2020-08-27
dc.description.abstractUtafiti huu ulichunguza uundaji wa vitambulisho vya utaifa katika tamthilia ya Mstahiki Meya, Arege (2009).Tamthilia ni kazi ya kidrama na ya kimaongezi ambayo huigizwa mbele ya hadhira au ni kazi iliyoandikwa ili kusomwa na hadhira. Isitoshe maagizo haya huakisi hali halisi katika jamii. Lengo kuu la kutunga tamthilia ni kuadilisha na kuwawezesha wananchi kutambua baadhi ya mambo yanayotendeka katika jamii halisi kwa kuwa, fasihi ni ukweli wa maisha. Vitambulisho ni sifa, hisia ama imani ambazo humtofautisha mtu au kabila au raia wa nchi fulani na nyingine. Huku utaifa ni hali ambapo wananchi wote hujitambua kuwa sawa katika taifa fulani na hushiriki kwa pamoja katika kuleta amani na maendeleo taifani mwao.Utafiti huu ulinuia kujibu swali lifuatalo, Kwanza, dhana ya vitambulisho vya utaifa vimejitokezaje kwa mujibu wa tamthilia ya Mstahiki Meya? Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhistoria mpya ikishirikiana na nadharia ya utaifa. Umuhimu wa utafiti huu ni kwamba, utaongeza maarifa katika nadharia na mbinu za uhakiki wa tamthilia za Kiswahili nchini Kenya, kwa kurejelea na kuweka wazi vitambulisho vya utaifa, pia utaweza kutumika katika taaluma ya fasihi hususan tamthilia, kama marejeleo na itawasaidia wanafunzi na watafiti watakaotaka marejeo ya tamthilia ya Kiswahili nchini Kenya ili kuweka wazi vitambulisho vya utaifa na jinsi vinavyojitokeza katika tamthilia, vilevile ni malighafi kwani utatoa mchango mkubwa katika historia ya tamthilia nchini Kenya na kutajirisha maktaba ya chuo kikuu cha Kisii. Aidha, tume ya utangamano wa taifa nchini Kenya (NCIC), itagundua umuhimu wa fasihi kupitia tamthilia, katika uundaji wa vitambulisho vya utaifa inayoendeleza utangamano nchini hivyo basi itawawezesha kufadhili tafiti zitakazonuia kushughulikia suala hili. Uchunguzi huu ulifanywa maktabani. Muundo wa utafiti uliotumiwa ni utafiti elezi. Kwa hivyo matokeo yaliwasilishwa kupitia maelezo
dc.identifier.citationVol. 4 No. 1 (2020)
dc.identifier.issn2520-3991
dc.identifier.otherhttps://doi.org/10.47672/ajep.560
dc.identifier.urihttps://indexedjournals.org/handle/123456789/1000
dc.language.isoen
dc.publisherAJPO
dc.titleUchunguzi wa Uundaji wa Vitambulisho Vya Utaifa Katika Tamthilia ya Mstahiki Meya
dc.typeArticle

Files

Original bundle

Now showing 1 - 2 of 2
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Journal of Education and Practice.jpg
Size:
41.49 KB
Format:
Joint Photographic Experts Group/JPEG File Interchange Format (JFIF)
Loading...
Thumbnail Image
Name:
560-Article Text-2006-2237-10-20200827.pdf
Size:
595.39 KB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed to upon submission
Description: